Latest Updates

Tanzia: Muongozaji wa filamu na vipindi vya TV George Tyson Afariki kwa ajali ya gari


Msiba mkubwa umeikumba tasnia ya filamu na habari Tanzania, George Tyson muongozaji mkongwe wa filamu za Tanzania na vipindi vya Television amefariki dunia jana usiku (May 30) baada ya kufuatia ajali mbaya ya gari.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa chanzo kilichokuwa kwenye eneo la ajali hiyo, marehemu na timu ya kipindi cha television cha The Mboni Show walikuwa wakitoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam lakini kwa bahati mbaya gari alilokuwa amepanda aina ya Noah lilipata pancha katika matairi mawili ya upande wa kushoto na kupinduka.
George Tyson alikuwa miongoni mwa watu wanane katika gari hilo, lakini yeye pekee ndiye aliyepoteza maisha.
Watu mbalimbali wameupokea taarifa za msiba huo kwa mshituko mkubwa.
Monalisa ambaye ni mtangazaji wa 100.5 Times Fm, ambaye marehemu George ni baba wa mtoto wake aitwae Sonia, na aliwahi kuwa mke wa ndoa wa marehemu,  ameandika ujumbe mzito wenye majonzi na kupost picha kwenye Instagram..
“George,u were my 1st director,then my friend, you became my lover,then hubby,then the father of my 1st born Sonia Akinyi,then you turned out to be my enemy,then back to be mabeste.leo umeniweza. SONIA your angel as you always call her haamini hadi sasa.nalia kwa nguvu,nalia moyoni,nina maumivu ya ajabu.RIP George Otieno Okumu.” Ameandika Monalisa kwenye Instagram.
100.5 Times Fm imeguswa na msiba huu kwa kuwa alikuwa mtu wa karibu kwa watangazaji na wiki moja iliyopita alikuwa akifanya kazi kwa karibu na Times Fm kama muongozaji wa vipindi wa TV1 na kupromote vipindi vya kituo hicho cha runinga.
“Pole kwa ndg jamaa na marafiki hakika msiba mwingine mkubwa sana juzi alikuepo @timesfmtzwakati anasepa akantania mwanagu unatoka saa 5 usiku we mfanya kazi bora nini? Dah kumbe few days to go...pole @monalisatz n #sonia ..tujiandaen hatujui siku zetu.” Ameandika Jabir Saleh, 

0 Response to "Tanzia: Muongozaji wa filamu na vipindi vya TV George Tyson Afariki kwa ajali ya gari "

Post a Comment