Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu akiwa ameshikiriwa na watu wa huduma ya kwanza mara baada ya kutoka kuaga mwili wa msanii mwenzao.
Msanii wa filamu nchini Jb akiwa yupo katika hali ya huzuni mara baada ya kutoka kuaga mwili wa marehemu
IMEGUNDULIKA kuwa wasanii wa Nyanja mbalimbali nchini wanafanya kazi katika mazingira magumu hali inayowapelekea kushindwa kupata nafasi ya kuchunguza afya zao.
Hayo yalizungumzwa na Waziri wa Habari vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fennella Mukangara wakati wa kuaga mwili wa msanii wa filamu nchini Adamu Kuambiana katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ambapo waziri huyo ameweka wazi kuwa wasanii hao wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na hali ilivyo ngumu katika soko la Sanaa nchini.
Huku akibainisha kuwa bado jamii haijagundua thamani ya kazi hiyo, kwani ni kazi ngumu kazi hiyo ni nzito ambayo inahitaji kujipangilia na muda wa kufanya kazi hiyo.
Pamoja na hayo amewataka wasanii kujitunza, kujilea na kukumbuka kwenda hospitali kwa ajili ya kuchunguza afya zao pindi wanapojisikia hali yao si nzuri.
Huku akitoa wito kwa wasanii kujiunga na huduma ya afya ili iwe rahisi kwao kujihudumia, pamoja na hayo aliwataka wasanii hao kujitunza kwani wao ni kioo cha jamii.
SIKILIZA HAPA LINK
0 Response to "AUDIO: YALIYOJILI KATIKA MAZIKO YA MSANII ADAM KUAMBIANA "
Post a Comment