Muigizaji Brad Pitt alijikuta katika wakati mgumu Jumanne iliyopita katika uzinduzi wa filamu mpya ya mchumba wake Angeline Jolie inayoitwa ‘Maleficent’, baada ya kupigwa usoni na ripota wa TV ambaye ni raia wa Ukraine.
Ripota hiyo kazi yake kubwa katika TV ni kuwatania kwa vitendo watu maarufu kwa kupanga matukio na kisha kurekodi na kuonesha jinsi wanavyo-react (Prankster).
Hata hivyo, ripota huyo aliyetajwa kwa jina la Vitalii Sediuk, hakuonesha nia ya utani wakati wakiwa katika red carpet baada ya kuupenya umati na kumpiga usoni Brad Pitt na kuvunja miwani yake ya jua.
Walinzi waliingilia kati na kumdhibiti Sediuk na kisha kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
Vyombo vya usalama vimetoa amri ya dharura ili kumlinda Brad Pitt na amri hiyo inamtaka Sediuk kukaa mbali na Brad Pitt, umbali usiopungua hatua 500 kwa muda wa siku tano zijazo.
Ripota huyo mwenye umri wa miaka 25 amefanya tukio hilo wakati ambapo bado yuko kwenye kipindi cha matazamia (Probation) kwa tukio alilolifanya mwaka 2013 kutaka kuingilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Adele kwenye tuzo za Grammy.
Chanzo kimeiambia TMZ kuwa file la kesi yake limepele kwa muendesha mashitaka wa Los Angeles na kwamba anaweza kukabiliwa na kesi ya jinai.
0 Response to "Brad Pitt apigwa na 'ripota' kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya Angelina Jolie "
Post a Comment