Latest Updates

Wagosi Wa Kaya wamshirikisha Lady Jay Dee kwenye albam yao ya UAMSHO


Kundi la Wagosi Wa Kaya limerudi tena mwaka huu na linatarajia kuachia albam yao huku likiwa limezitanguliza nyimbo mbili zenye video tayari ambazo ni Bao na Gahawa.
Mwanafamilia wa kundi hilo, Mkoloni ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa albam hiyo imejaa nyimbo zitakazolilipa deni kubwa wanalodaiwa na mashabiki wao na kueleza kuwa katika albam hiyo kuna wimbo waliomshirikisha Lady Jay Dee 'Anaconda' kwa mara ya kwanza.
“Tumeshafanya wimbo mmoja na Lady Jay Dee ambao utakuwa kwenye albam ya Uamsho na tumefanya nae kwa sababu tunaamini ni mwanamuziki anaejitambua na anaeheshimika sana mbele ya jamii.” Amesema Mkoloni.
“Na pia amekuwepo katika tasnia hii ya muziki kwa muda mrefu, hivyo anao uzoefu wa kutosha na pia kuleta ladha kwa kuwa hatukuwahi kufanya nae kazi hata siku moja.” Ameongeza.
Hata hivyo, amesema ni mapema sana kutaja jina na studio waliofanyia wimbo huo.
“Yote yatajulikana kupitia tovuti hii na nyingine, kupitia ukurasa wetu wa Facebook ambao ni ‘Wagosi wa Kaya Tanzania’. Na radio mbalimbali ikiwemo radio Times Fm.

0 Response to "Wagosi Wa Kaya wamshirikisha Lady Jay Dee kwenye albam yao ya UAMSHO"

Post a Comment