Latest Updates

Ridhiwani Kikwete aeleza faida na hasara anazopata kwa kuwa mtoto wa Rais

Kama uliwahi kufuatilia zile hadithi za ‘hapo zamani za kale’ lazima uliona kila aliye kwenye simulizi hilo anatamani kuwa mtoto wa mfalme au malkia, lakini kwa nchi ya Kidemokrasia kama Tanzania nafasi hiyo tunaweza kuifananisha kidogo na kuwa mtoto wa rais wa nchi.
Ridhiwani Kikwete, mtoto wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chalinze aliongea na Sun Rise na kueleza faida anazopata kwa kuwa mtoto wa rais.
“Faida kubwa unayoipata nafikiri ni kuwa karibu na opportunities kubwa ambazo unaweza kuzipata katika maisha. Kwa maana ya kwamba unaposema ninataka jambo fulani kwako inaweza kuwa rahisi kulipata. Kwangu hiyo ndio faida kubwa ambayo mimi naiona.” Amesema Ridhiwani Kikwete.
Ridhiwani ameeleza kuwa yeye ameibadilisha faida hiyo ili kuwafaidisha watu wengine pia, “kwangu mimi nimei-turn hiyo kuona jinsi gani naweza kuwasaidia watu...kwangu mimi.”
Lakini hakuna chenye faida duniani kisichokuwa na hasara kwa upande wa pili, Ridhiwani pia anakumbwa na hasara ambayo anaamini inatokana na kuwa mtoto wa rais.
“Lakini hasara kubwa unayoipata ni watu wanaposhindwa kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani. Na wakati mwingine kukataa pia kukufahamu wewe ni mtu gani. Hiyo ndio hasara kubwa ambayo mimi binafsi ninayoipata.” Ridhiwani ameiambia Sun Rise ya Times Fm.
Hata hivyo, Ridhiwani ameeleza kuwa haoni tofauti yeyote ya kuwa mtoto wa rais na kuwa mtu mwingine yeyote, “Otherwise, naona hakuna tofauti ya kuwa mtoto wa rais na kuwa mtoto wa fulani. Kwa sababu inategemea tu jinsi mwenyewe unavyoichukulia hiyo nafasi yako.”
Kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu kamili asubuhi.
Unaweza kusikiliza online kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’

0 Response to "Ridhiwani Kikwete aeleza faida na hasara anazopata kwa kuwa mtoto wa Rais"

Post a Comment