Latest Updates

MASSELE CHA POMBE SASA YUKO FREEEEEE


                            Crispin Lyogello
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya Vichekesho aliyekuwa na mkataba na kundi la vituko Show Crispin Lyogello ‘Massele Cha pombe’ameweka wazi kuwa kwasasa hawezi kuchagua kundi la kufanya nao kazi kwasababu mkataba wake na Al – Riyamy umeisha na ana uwezo wakufanya kazi popote anapotaka.
Masele ambaye alijibebea umaarufu kutokana na umahiri wake na ubunifu wa kucheza kama mlevi kupita kiasi katika sanaa yake ya vichekesho alisema kuwa kipindi cha nyuma hakuweza kufanya kazi kwenye kampuni nyingine kwasababu alikuwa na mkataba na kampuni ya Al-Riyammy lakini kwa sasa mkataba wake umeisha na ameamua kufanya kazi nje ya kampuni hiyo mpaka atakapoamua kurudi tena.

“Nilikuwa nimesaini mkataba na Kundi la Vituko Show lakini kwasasa mkataba umekwisha nafanya kazi zangu mwenyewe sijabahatika kupata kampuni ya kufanya nao kazi,siyo kama sito rudi kwenye kundi langu la zamani naweza kurudi lakini kwa sasa ngoja nifanye kazi zangu mpaka nitakapo pata kampuni nyingine ya kufanya nayo kazi.
             Crispin Lyogello
“Mfano sasahivi nipo Dar es Salaam kunakipindi natengeneza kinahusiana na katiba kitakua kinachekesha lakini kinaelimisha na ndiyo maana nikasema watu wasije wakahofia kuwa wakinihitaji kufanya kazi na mimi nitakataa,”anasema Masele.

Msanii huyo amesema kuwa hapo awali ilikuwa ngumu kufanya hivyo kwani alikuwa chini ya Al- Riyamy Production, kwa sasa yupo free kufanya kazi na msanii au kampuni yoyote itakayomhitaji.

0 Response to "MASSELE CHA POMBE SASA YUKO FREEEEEE"

Post a Comment