KUNDI la Wagosi wa Kaya ambalo lilikaa kimya kwa muda wa miaka 8 hivi sasa lipo katika mikakati ya mwisho ya kuandaa albamu yao huku wakiwa karibu na mashabiki yao ikiwa ni njia moja wapo ya kutumia mitandano ya kijamii ili kuweza kuliteka soko la burudani.
Katika kutumia njia ya mitandao ya kijamii kama moja wapo ya kuwa karibu
na mashabiki wao kundi hili kupitia ukurasa wao wa Facebook ili
wapendekeza majina ya wasanii ambao mashabiki wao wangependa kufanya nao
kazi.
Baada ya kuomba mashabiki wawapendekeze ni wasanii gani ambao wangependa
wafanye nao kazi ya muziki ikiwa ni nimbo moja ya kushirikiana.
Baada ya kupendekeza juzi, kundi hilo lilitoa matokeo kwa mashabiki wao
huku ikionesha kuwa Juma Nature, pamoja na Roma ndio wasanii
waliopendekezwa kwa wingi na baadhi ya mashabiki wao kufanya nao kazi ya
muziki.
Kupitia ukurasa wao wa Facebook kundi hilo liliandika kuwa "wasanii
ambao wamependekezwa sana ili tufanye nao kazi katika nyimbo ni pamoja
na Juma Nature, Roma na wengineo wengi tu, naamini hatujawahi kufanya
kazi na wasanii wengi ila kwa heshima yenu mashabiki tutashirikiana na
hao mliowachagua na wengineo tutashirikiana nao na mtawasikia kwenye
alamu yetu ya uamsho hatutawaangusha kamwe".
0 Response to "WAGOSI WA KAYA KUSHIRIKIANA NA JUMA NATURE, ROMA"
Post a Comment