
MWANAMUZIKI nyota wa miondoko ya Hip Hop Jay Z ambaye pia ni rafiki wa karibu na bwana harusi mtarajiwa Kanye West, imedaiwa kuwa hatohudhuria katika ndoa ya rafiki yake huyo ambayo inatarajiwa kufungwa hivi karibuni.
Sababu zinazopelekea Jay Z pamoja na mke wake kutohudhuria ndoa hiyo ni
kutokana kwa sherehe hiyo kuoneshwa kwenye kipindi cha reality show ya
Kim Kardashians ambaye ndiye mwanamke anayetarajia kufunga ndoa na
Kanye.
Ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa mwezi ujao jijini Paris Ufaransa chanzo
kimoja kimedai kuwa Jay Z tayari ameshampa taarifa rafiki yake huyo kuwa
yeye pamoja na familia yake hawataudhuria sherehe hiyo kutokana na
sababu hizo.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun limedai kuwa Jay Z amepanga kuwafanya
sherehe kubwa mara baada ya tukio hilo kumalizika ambapo sherehe hiyo
ameipanga kuifanya New York ndani ya ukumbi wa 'Club 40/40.
0 Response to "JAY Z KAWAANDALIA ZAWADI NONO KANYE WEST NA KIM"
Post a Comment