Latest Updates

50 CENT 'AMCHANA' KANYE WESTKIONGOZI wa kundi la  G-Unit, 50 Cent adai kuwa hapendezwi na albamu ya Kanye West inayojulikana kwa jina la ‘Yeezus’ huku akiweka wazi kuwa albamu inayomvutia zaidi ni ile iliyotolewa na mwanamuziki huyo mwaka 2004 inayojulikana kwa jina la  ‘The College Dropout’.

50 Cent alitongea hivyo katika mahojiano na MTV News ya U.K kuhusu albam hiyo ambapo aliweka wazi kuwa yeye husikiliza zaidi albamu ya mwaka 2004.

Alisema kuwa Kanye West ni mtu mwenye kipaji kikubwa katika utamaduni wa Hip Hop, huku akiweka wazi kuwa ni mmoja ya watu wanaousogeza muziki wa Hip Hop duniani kote.
Mbali na hayo alisema ingawa Kanye ni kapaji lakini kuna baadhi ya vitu vingine anavyofanya vya ajabu ambapo rekodi yake ya mwisho hapendi kuisikiliza kutokana na kile alichokuimba kukosa ubunifu.
"Nikizungumza ukweli ni kuwa albamu yake ya mwisho siisikilizi bado ninapata nafasi na ninajisikia vizuri zaidi endapo nikiisikiliza rekodi yake ya mwaka 2004 katika albamu yake hiyo ameweza kufanya vitu vipya vya kibunifu zaidi kuliko hii ya sasa" alisema 50 Cents.

0 Response to "50 CENT 'AMCHANA' KANYE WEST"

Post a Comment