LICHA ya kutawala kwa ukimya wa muda mrefu kwa mwanamuziki maarufu wa
miondoko ya Kikongo, Koffi Olomide amedhihirisha mashabiki wake kuwa
bado yupo katika gemu hilo ambapo aliweza kufanya show ya nguvu nchini
Uganda huku akiwapagawisha mashabiki wake.
Olomide alifanya show hiyo mwishoni mwa wiki nchini humo hali
iliyopelekea mashabiki kumkubali na kutaka kurudia nyimbo zake kali
zilizowahi kutamba miaka ya 90 iliyopita.
Hali hiyo imedhihirika kuwa mwanamuziki huyo hajachuja hata kidogo licha
ya ukimya wake wa miaka mingi baada ya Mashabiki kubaki wakitaka zaidi
katika shoo ya kukata na shoka .
Mwanamuziki huyu wa miondoko ya soukous, ambaye pia ni mcheza show,
mtayarishaji Muziki na Mtunzi alikonga nyoyo za mashabiki baada ya
kuwapa zaidi ya walichokuwa wakitarajia katika onyesho ambalo lilikua
maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kujenga maabara kwa ajili ya
damu salama nchini Uganda iliyoandalia na klabu ya Rotary.
Kabla ya Koffi kupanda stejini alipanda mwanamuziki kutoka Canada,
mlemavu wa Mikono ambaye alipiga ngoma kwa kutumia miguu yake huku
akiwaacha maelfu wa mahabiki midomo wazi na kuufanya usiku ule kuwa
usiku wa kihistoria Jijini Kampala.
0 Response to "KOFFI OLOMIDE APAGAWISHA UGANDA"
Post a Comment