Latest Updates

DIAMOND ASHINDWA KUZUIA HISIA ZAKE, ATOKWA NA MACHOZI


IMESIBITISHWA kuwa wimbo ulioimbwa na msanii wa muziki nchini Profesa Jay aliomshirikisha Diamond Platinumz ‘Kipi Sijasikia’umepokelewa kwa hisia za tofauti na mashabiki wengi ambao wengi wao wameguswa na ujumbe kwa madai kuwa kile kilichoimbwa kimegusa maisha yao moja kwa moja.
Akizungumza katika mahojiano maalumu katika radio ya TIMESFM, Profesa Jay ameweka wazi nyimbo hiyo imegusa watu wengi hali iliyopelekea kupigiwa simu na baadhi ya mashabiki huku wakimwambia kuwa nyimbo hiyo ipo kwa ajili yao.

Aliweka wazi kuwa kiitikio cha wimbo huo pia kinaongeza hisia kali kwa watu ambao ujumbe unawahusu hali iliyopelekea Diamond kutokwa na machozi pindi alipokuwa akiimba kiitikio hicho.
Alisema Diamond Platinumz alijikuta akitokwa na machozi akiwa studio alipokuwa akiimba nyimbo hiyo ambapo alishindwa kuzuia hisisa zake kutokana na kiitikio hicho kilivyokuwa kimebeba ujumbe.
Profesa aliiambia Sun Rise ya Times Fm kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo alikuwa analia kutokana na kuguswa na ujumbe wa wimbo huo pamoja na kufanya kazi na wakongwe Profesa Jay na producer Majani.

“Lakini kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond analia. Alikuwa imotional unajua ile...ilimgusa sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na Majani ‘huyu jamaa analia nini?’

0 Response to "DIAMOND ASHINDWA KUZUIA HISIA ZAKE, ATOKWA NA MACHOZI"

Post a Comment