UBOVU WA MITARO KITUO CHA MABASI MWENGE NI KEROO JIONEE
Hii
ni sehemu ya maduka ambayo kwa mbele ya hayo maduka maji yamejaa
kutokana na kuziba kwa mitaro ya eneo la stendi ya daladala ya Mwenge
jijini Dar es salaam
Sehemu
hii kuna mtaro wa maji lakini kutokana na kuziba kwake imekuwa kero kwa
wafanyabiashara na watu wanaotumia stendi ya Mwenge kwani mitaro hiyo
imeziba na kupelekea maji kujaa na kuingia barabarani hata madukani.
Maji
ya mvua yakiingia kwenye mtaro wa maji ambao kwa mbele kumezibwa
kutokana na uchafu ulioko kwenye mtaro huo wa stendi ya Mwenge
Hii ni sehemu ya mtaro mmojawapo ambao unapokea maji mengi pale mvua inaponyesha lakini hayawezi kwenda kwani pameziba.
Eneo
hili ndipo daladala zinapoingilia kwenye kituo cha Mwenge kilichopo
Kinondoni. Eneo hili halipitiki wakati wa mvua ikinyesha kutokana na
mitaro mingi kuziba na kujaa maji mengi ndani ya stendi hii.
Sehemu
hii pameja maji lakini kwa chini kuna mtaro mkubwa ila kutokana na
kuziba inapelekea maji kujaa sehemu kubwa ya maduka na hata barabarani.
Unaweza kusema ni mto lakini kumbe ni maji ya mvua yaliyotuhama kutokana na mitaro kuziba
Hii ndio hali halisi kama inavyoonekana katika picha
Kutokana
na kuziba kwa mitaro hiyo maji yanaingia mpaka kwenye barabara ya
Bagamoyo inayopita karibu na kituo hicho cha Mwenge.PICHA NA PAMOJA BLOG
0 Response to " "
Post a Comment