

Sehemu
ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakitawanyika mara baada ya
mwenyekiti kuahirisha kikao kutokana na baadhi ya wajumbe kutoelewana
katika hoja.

Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ole Sendeka akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu tuhuma za baadhi ya wajumbe kuwa Mwenyekiti anampendelea
kwa kumpa nafasi nyingi za kuchangia hoja katika semina ya kanuni za
bunge maalum.

Mjumbe
wa Bunge la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo,Mhe. Freeman Mbowe akiongea na waandishi wa habari nje ya
Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,mara baada ya kuahirishwa kwa kikao.

Mjumbe
wa Bunge la Katiba,Mhe. Kajubi Mkajanga kutoka taasisi ya vyombo vya
Habari akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwemyekiti
kulazimika kiuahirisha semina ya kujadili kanuni hadi saa kumi na moja
(11:00) jioni.
Semina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba leo imelazimika kuahairishwa baada ya kuibuka vurugu ndani ya ukumbi wa Bunge.
Zogo
hilo liliumuka baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya wajumbe
uliosababishwa na kutuhumiana kwamba zipo dalili za upendeleo
wanazofanyiwa baadhi ya wajumbe kutokana na sababu za kiitikadi za
vyama.
Hali
hiyo ya hewa ilichafuka baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya Mjumbe
Mhe. Christopher Ole Sendeka ambaye aliingia katika mvutano na Mjumbe
wa Kamati ya Kanuni Mhe Abubakar Hamis Bakari kuhusiana na uwasilishwaji
wa majedwali ya marekebisho ya kanuni.
Awali
Mjumbe Sendeka alipewa ruksa na Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo Mhe
Pandu Ameir Kificho, awasilishe mapendekezo ya mabadiriko katika
kifungu cha 58 cha kanuni hizo kilichokuwa kikijadiliwa muda huo.
Lakini
baada ya Mhe Sendeka kuwasilisha mabadiriko yake, alisimama Mjumbe
Bakari ambaye kiutaratibu alipaswa kujibu hoja hiyo hasa kwa kuwa ni
mjumbe wa kamati ya kanuni.
Mhe.
Bakari alikataa kupokea hoja ya mabadiriko ya Mhe. Sendeka kwa kusema
kuwa hayakuwa yamewasilishwa kwa kufuata taratibu za uwasilishwaji wa
mabadiriko ya majedwali, na kwamba Kamati haina mapendekezo hayo hivyo
haiwezi kujibu jambo lisilo jadiliwa.
Katika
kukataa huko Bakari alikitupia lawama kiti cha Mwenyekiti huyo kwa
madai kuwa kimekuwa kikitaja majina ya wajumbe na kuwapa nafasi ya
kuongea wakati hawapo kwenye utaratibu wala hawakuwa wameomba toka
awali.
Aliongeza
kuwa si kwa Mhe. Ole Sendeka pekee, bali pia Mwenyekiti huyo amekuwa
akiataja wajumbe wengine wakiwamo Peter Serukamba pamoja na Umy Mwaimu
ambao wote hawakuwa wamewasilisha majedwali ya mapendekezo ya
marekebisho toka awali.
"Mheshimiwa
Mwenyekiti, Ole Sendeka hayupo katika orodha ya walioleta mapendekezo,
lakini nashangaa wewe unampa nafasi ya kuzungumza wakati hakuwapo kwenye
orodha yetu, kamati hatuwezi kumpa nafasi ya kujibu hoja yake
hatuitambui.
"Hata
hao wakina Ummy Mwalimu hawapo katika orodha. Mwenyekiti ukiendeleza
huu mtindo wa kuruhusu kila anayetaka kuzungumza hapa azungumze
hatutofika. tutatumia miezi 6 hapa kutengeza kanuni tu. Lazima uwe na
maamuzi kuwa wanaoleta mapendekezo hivi sasa hatupokei"alisema Mhe
Bakari
Baada
ya Mhe Bakari kumaliza kuzungumza, Mhe Kificho aliingilia kati na
kusema kuwa jambo hio linaweza kuwa limechanganywa na sekretarieti
inayoandaa na kwamba yeye binafsi amepewa majina ya waliopeleka
marekebisho hivyo anashangaa kuona kama hayapo kwa wajumbe hao.
Mhe
Kificho alitoa ruksa kwa Ole Sendeka kuongea tena, ambapo katika
mazungumzo yake alitoa kaulia akisema kuwa mapendekezo yake
aliyawasilisha mapema na kwamba kama Mhe Bakari ana itikadi zake za
vyama asimuhusishe humo.
Mhe.
Ole Sendeka alisema kuwa yeye ana uzoefu wa kanuni na kwamba alifuata
taratibu akiwa na wenzakeMhe Serukamba pamoja na Mhe Mwalimu na kwama
kama mapigo yao yanawaumiza wajumbe wengine wavumilie tu.
"Mheshimiwa
mwenyekiti tuliopo hapa ni wajumbe. Nilijua na mimi sio dhaifu kwenye
kanuni. Nnajua haki yangu kwa kuwasilisha kwa wakati, nilitimiza wajibu
wangu, kama mapigo yetu yanawaumiza.
"Kazi
yetu si kupeleka majina yetu kwa Abubakari, kama yeye ana chama chake
na hoja zetu zinamuuma, asimame na kutuweka wazi kuwa yupo katika
msimamo gani. Lakini mimi nimewasiisha kama taratibu
zinavyonitaka"alisema Ole Sendeka
Kauli
ya Mhe Sendeka ilianzisha sintofahamu ndani ya Bunge hilo baada ya
baadhi ya wajumbe kuanza kuzomea na wengine wakisiama na kutaka kupewa
ruksa ya kuzungumza huku wakiwasha vipaza sauti.
Hali
hiyo ilimuinua Mhe Kificho ambaye aliwasihi wajumbe kuacha kuingiza
masuala ya vyama hasa kwakuwa wajumbe walioingia hapo ndani
wamewakilisha makundi.
"Niwaombe
wajumbe tujitahidi sana, tusionyeshe misimamo ya vyama, tumepata
heshima kubwa ya kuwapo humu ndani hivyo si vyema kuanza kuonesha vidole
kwasababu huyu katika CCM, sijui CUF ama Chadema au kokote itaibua
hisia ambazo si vyema.
"Mheshimiwa
Ole Sendeka naona ulimi umekwenda mbali kidogo ukamgusa mheshimiwa
Bakari. Mimi naona hili jambo limekwenda nje. Kwa hiyo naomba tuwe
makini"alisema Kificho
Baada ya kauli ya Kificho, wajumbe walianza kupiga kelele wakitaka Mhe
Ole Sendeka kumwomba radhi Mjumbe Bakari huku wengine wakimtaka asifanye
hivyo.
Mhe
Kificho alitoa nafasi nyingine kwa Mhe Bakari kuzungumza, ambapo
katika mazungumzo yake ndipo fujo hizo zilipoibuka.
Katika Mazungumo yake, Mhe Bakari alisema kuwa alichosema yeye ni kwa
faida ya Bunge na nchi, na kwamba taratibu ni kuwasilisha mapema
mapendekezo na kwamba majina ya kina Sendeka hayakuwapo.
"Mimi
nilizungumza vizuri hili kuweka utaratibu mzuri wa kupokea majedwali
haya. Mheshimiwa mwenyeiti kwa bahati mbaya mdogo wangu Ole Sendeka
anadai kanuni anazijua vizuri, lakini ninachosema sifikirii..sifikirii
kama ana uzoefu wa kujua kanuni kunishinda mimi.
"Mheshimiwa
mwenyekiti toka mwaka 1980 nipo katika mabunge haya, kwa hivyo
sifikirii kama mtu katoka Simanjiro miaka kumi iliyopita anaweza akaja
hapa na kusema anajua kanuni kunizidi.
"Mimi sitaki aniombe radhi, ila ninachotaka kumfahamisha ni kwamba kuna
watu wana ujuzi zaidi kuliko yeye hivyo awe makini katika mazungumzo
yake"alisema Bakari
Kauli hiyo ilizidisha mgawanyiko katika Bunge hilo, ambapo wajumbe walisimama na kuanza kupiga meza wengine wakizomea.
Baadhi ya wajumbe walionekana wakirushiana maneno na hata kupeleka kutaka kurushiana makonde.
Hali
hiyo ilipeleka askari ambao ni wapambe wa Bunge kusogea karibu ikiwa ni
njia ya kutuliza vurugu hizo, huku wajumbe hao wakiendelea kurushiana
maneno.
Vurugu
hizo zilionekana kusambaa katika ukumbi mzima ambapo wajumbe wengine
walionekana kurushiana maneno, hali iliyopelekea Mhe Kificho kuahirisha
Semina hiyo.
NA MICHUZI BLOG
Wabunge
wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma Machi 6, 2014
baada ya Bunge hilo kusitihwa kwa muda kufuatia Sitofahamu iliyotokea.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif
Idd (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa muda Machi 6,2014 Ajali yaua saba, 11 hoi
Watu saba wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa baada
ya basi la dogo aina ya Nissan Civilian walilokuwa wakisafiria
kugongana uso kwa uso na lori katika barabara kuu ya Chalinze- Segera
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo cha Chalinze Mzee jirani na kwamba majeruhi tisa kati yao ni mbaya.
Kamanda Matei alisema basi hilo lenye namba za usajili T573 CQD likitokea Msata kwenda jijini Dar es Salaam liligongana na lori hilo lenye namba T921 BFD/T 470 BFY wakati likitoka Chalinze kuelekea Tanga.
Kamanda Matei aliwataja waliokufa kuwa ni Dege Ally, Tunu Said Khalfan, Tumaini Hussein, Jafar Suleiman, Emmanuel David na wawili ambao majina yao hayajafahamika.
Kadhalika, Kamanda Matei aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni dereva wa basi hilo, Ndege Ally, kondakta wake, Deo Mosses, Bitela Msuha, Zaina Mkombozi, Salumu Idd na Chadugu Paulo.
Wengine ni Abdul Wela ambaye ni mwanafunzi darasa la kwanza shule ya Kwaifugo Mkata, Geoffrey Anthony, Juma Athuman, Shaban Omar ambaye ni dereva wa lori na Shoshy Mohamed ambaye ni utingo wake na majeruhi wengine bado majina yao hayajatambulika.
Kwa mujibu wa Kamanda Matei, majeruhi wengi wa ajali hiyo wameumia vibaya sehemu za miili yao na wapo waliovunjika miguu na mikono na wote kupelekwa Kituo cha Afya Chalinze kupatiwa matibabu.
Kamanda huyo ambaye alifika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali hiyo, alisema kuwa chanzo chake hakijajulikana na kwamba uchunguzi unaendelea.
Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Victor Bamba alisema kuwa wakati ajali hiyo ikitokea, watu watano walikufa papo hapo na wengine 13 kujeruhiwa.
Dk. Bamba alisema wakati wakikimbizwa kwenye kituo hicho cha afya mmoja alifia njiani na mwingine kituoni hapo wakati akipatiwa matibabu.
Alisema watu hao wawili waliokufa walikuwa miongoni mwa majeruhi tisa waliokuwa mahututi kutokana na kujeruhiwa vibaya baada ya ajali hiyo kutokea.
Alisema majeruhi waliosalia walihamishiwa walihamishiwa katika hospitali Teule ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi iliyopo wilayani Kibaha.
NIPASHE lilipofika Tumbi, mwandishi hakuruhusiwa kuingia wodini kwa maelezo kwamba ni lazima aruhusiwe na Ofisa Habari, Gelard Chami, ambaye hata hivyo alikuwa kwenye kikao.
Baadaye Chami akizungumza kwa simu jioni alithibitisha kupokelewa kwa majeruhi hao kati ya hao usiku wa manane jana.
Alisema kati ya hao, sita walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na wengine wanaendelea na matibabu kutokana na hali zao kuwa mbaya.Chami alisema kuwa wawili kati ya hao wanatarajia kufanyiwa upasuaji mkubwa.
MASHUHUDA
Hata hivyo, kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, Hussein Halfan na Yusufu Hussein, ajali hiyo ilitokana na uzembe wa dereva wa Nissan kwani ilikuwa ikiongozana na Toyota Hiace na ilipofika eneo hilo, Hiace ilitoka upande wa kulia wa barabara na kuyapita malori waliyokuwa mbele yake na dereva wa Nissan aliifuata Hiace bila kusubiri lori lililokuwa mbele na hivyo kukutana nalo uso kwa uso.
CHANZO:
NIPASHE
0 Response to "TAZAMA PICHA ZA VURUGU BUNGENI LEO NA TAARIFA KAMILI KUHUSU MZOZO ULIOTOKEA"
Post a Comment