HATIMAYE kifungu cha 57 fasihi ndogo ya 3 inayozungumzia
nafasi ya waandishi wa habari kuruhusiwa kuingia katika vikao vya kamati ya
Bunge Maalum la Katiba
imepitishwa na wabunge wa CCM huku wabunge wa Chadema
akiachwa pasipo kujua cha kufanya.Hatua hiyo ni sawa na waandishi wa habari
kuchinjiwa
Habarini huku wananchi wakinyimwa uhuru wa kupata habari
kuhusu mambo yatakavyo endelea ndani ya vikao vya Bunge hilo.
Katika kile kinacho onekana kwamba ni njama za kuweka mambo
katika hali ya usiri zaidi, katika mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Mpya
inayoendeloe mjini Dodoma
inaonyesha ni jinsi gani wabunge wa CCM walijipanga kufanya
mambo kwa usiri na kuwanyima wananchi fulsa ya kujua mambo yanavyo endelea
ndani ya vikao vyao
Akizungumzia suala hili Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya
rasimu za kanuni za bunge hilo George Simbachawene alipinga suala hilo kwa
nguvu zote huku pia
akipingana hata na maamuzi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Professa Costerick Mahalu ambaye alitaka suala hilo liachwe wanza
ili kamati yake ikaangalie namna nzuri ya kuwaruhusu wanahabari kuingia katika
vikao hivyo.
Kitendo cha Simbachawene kushikilia msimamo huo inaleta
tafisiri kwamba huo ndiyo mpango wa Chama Cha Mapinduzi uliokuwepo tagu mwanzo
ya kuwataka wabunge wake
walijipange kufanya mambo yanayopaswa kuwa siri yafanyike
kwa uwazi na yake yaliyopangwa kufanyika kwa uwazi yafanyike kwa usiri bila
kujali kwamba wanavunja Katiba mama ambayo bado inatumika mpaka hivi sasa
Hoja za kuitaka bunge hilo kufuta mapendekezo ya kanuni
katika kifungu cha 51 na 57 fasiri ndogo ya 3 inayompa mwenyekiti wa kamati
haki ya kutoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari juu kilichozungumzwa na kamati, badala
ya kuruhusu waandishi waingie na kusikiliza kinachojadiliwa wenyewe na
kuwaeleza
wananchi wengine ilipigwa na Wabunge Halima Mdee Chadema
,Amos Machari NCCR-Mageuzi,Ester Bulaya CCM,Maria Sarungu na Ezekiel Oluoch wote
wateule wa Rais Kikwete.
0 Response to " "
Post a Comment