“Hata shughuli za kilimo zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo.”Dk Agnes Kijazi.PICHA|MAKTABA
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetabiri kuwa mvua kubwa zitanyesha
hasa maeneo ya ukanda wa pwani huku ikitahadharisha uwezekano mkubwa
kusababisha maafa.
Mkurugenzi
Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema jana kuwa utabiri huo unaonyesha
kuwa maeneo mengi zaidi ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za juu ya
wastani... “Hata shughuli za kilimo zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia
ushauri wa wataalamu wa kilimo.”
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari TMA pia imewahadharisha watumiaji wa
bahari juu ya mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kusababisha bahari
kuchafuka.
Taarifa
hiyo imesema kunatarajiwa kuwapo kwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi
milimita 50, kati ya jana na kesho ambazo zitanyesha mfululizo na kwamba
huenda zikasababisha madhara katika ukanda wote wa pwani.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa mvua hizo zinasababishwa na kuimarika kwa mgandamizo
mdogo wa hewa Mashariki mwa Bahari ya Hindi, sanjari na kusogea haraka
kwa mvua za masika hivyo kuongeza kiwango cha unyevunyevu kuelekea
ukanda wa pwani.
Mikoa
iliyopo katika ukanda huo ambayo inaweza kuathiriwa na mabadiliko hayo
ya hali ya hewa ni Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na
Zanzibar.
“TMA
inazitaka mamlaka zinazohusiana na majanga kuchukua hadhari
zinazostahiki ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua
hizo,” ilisema taarifa hiyo.
0 Response to "HALI YA HEWA YATABIRI MVUA ZA MAAFA PWANI"
Post a Comment