Latest Updates

Karrueche Tran alimuacha rasmi Chris Brown baada ya kumtembelea Rehab


Mwanamitindo Karrueche Tran ameweka wazi kuwa alimuacha rasmi Chris Brown baada ya kumtembelea alipokuwa Rehab akipata matibabu ya kudhibiti hasira baada ya kuamriwa na mahakama.
Kwa mujibu wa TMZ, Karrueche alienda Rehab February mwaka huu na alipoishika simu ya Chris Brown alikuta imejaa SMS za wasichana zenye jumbe za mapenzi.
Mrembo huyo ambaye anaelezwa kuwa alikuwa anampa sapoti Chris Brown kwa moyo wake wote wakati wa matatizo, aliumizwa na jumbe hizo na akaona ni bora kuendelea na maisha yake na kuachana na mwimbaji huyo.
Mapema mwezi huu, Chris Brown alifukuzwa Rehab kwa madai kuwa alivunja amri aliyopewa ya kukaa umbali wa futi kadhaa na mwanamke yeyote.
Amri hii ilitolewa kwa kuwa bado alikuwa chini ya Probation ya kesi ya kumpiga Rihanna mwaka 2009, lakini pia alisemekana kujihusisha na mapenzi akiwa ndani ya jengo hilo la Rehab.
Mwimbaji huyo wa Fine China hivi sasa yuko jela jijini Los Angeles hadi April 23 kesi yake itakaposikilizwa tena.

0 Response to "Karrueche Tran alimuacha rasmi Chris Brown baada ya kumtembelea Rehab"

Post a Comment