Latest Updates

Barack Obama na mkewe kuchora tattoo inayofanana, wapanga kupost picha zao


Raisi wa Marekani, Barack Obama ameeleza kuwa kama watoto wao Malia na Sasha hawataamua kuchora tattoo kwenye miili yao, yeye na mkewe Michelle Obama watachora tattoo zinazofanana hivi karibuni na kuzichukulia kama tattoo za familia.
Obama ameeleza wakati akifanya mahojiano na Ellen DeGeneres na kueleza kuwa watafanya hivyo ili familia yake yote iwe na tattoo zinazofanana zikiwa zimechorwa sehemu moja na kwamba wataonesha picha hizo kwenye mitandao.
“Michelle na mimi tutakuwa pale na tutapost picha ili kila mtu aweze kuona, tutakuwa na tattoos zinazofanana.” Amesema Obama.
Hii sio mara ya kwanza kusema hivyo, April mwaka jana Obama alimwambia maneno hayo mtangazaji wa kipindi cha ‘Today Show’, Savannah Guthrie kuwa aliwaambia wanae kuwa wasipochora tattoo yeye na mama yake watachora tattoo zinazofanana na wataweka kwenye Youtube.
“Kama nyie hamtaamua kuwa mtachora tattoo, mama na mimi tutachora tattoo zinazofanana, kwenye sehemu moja. Na tutaziweka kwenye YouTube na kuonesha kama tattoo ya familia.” Rais Obama alieleza kile alichowaambia wanae.

0 Response to "Barack Obama na mkewe kuchora tattoo inayofanana, wapanga kupost picha zao"

Post a Comment