Latest Updates

Christian Bella: Majungu, sifa na dharau zinaua bendi za dansi Tanzania



Member wa zamani wa bendi ya Akudo ambaye hivi sasa ni kiongozi wa bendi ya Malaika, Christian Bella ameeleza sababu zinazofanya bendi nyingi za Tanzania kusambaratika ama wasanii wake kutokaa pamoja.
Mwimbaji huyo ameiambia Tovuti ya Times Fm kuwa matatizo makubwa yanayopelekea bendi hizo kusambaratika ni pamoja na kusengenyana, majungu, kulewa sifa na dharau.
“Bendi hazidumu kwa sababu sisi vijana tunalewa sifa. Na pia kulewa sifa namaanisha kwamba kila mtu kwenye bendi ambayo tupo kwa style ambayo tunafanya Tanzania, katika bendi kila mtu anajiona ni star. Kwa sababu wewe ukiwekwa pale raisi wa bendi, bendi sio yako. Tofauti na Congo utakuta Koffi ndio mwenye band.” Ameeleza mwimbaji huyo kutoka Congo.
“Sasa wanamuziki wakishajua kuwa bendi sio yako kila mtu anajiwekaga star, halafu kuna dharau zinakuaga….kuna maisha ya kuishi unafiki. Hamna ile mapenzi ya kweli kwamba ushirikiano wa kweli.  Kunakuwa kuna majungu majungu. Asikudanganye mtu ndio zipo kwenye bendi zote ndio hizo zipo. Mkikaa wawiwi hivi mnavutana mnaua wale wawili.” Ameongeza.
Amefafanua kuwa dharau katika bendi zinachangia pia watu kushindwa kukaa pamoja katika bendi.

0 Response to "Christian Bella: Majungu, sifa na dharau zinaua bendi za dansi Tanzania "

Post a Comment