Latest Updates

C PWAA AFUNGUA RECORDING LABEL YAKEMSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini CPwaa, ameamua kuanza kuwasaidia baadhi ya wasanii chipukizi kwa kuanzisha 'recording label'yake binafsi aliyoipa jina la 'Brain Storm Music.
Msanii huyo ambaye ni mmoja kutoka kundi la  Parklane, teyari ameshaanza kufanya usajili wa wasanii mbalimbali kwenye label hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kwenye soko la muziki nchini.

Hayo aliyazungumza katika kipindi cha The Jump Off ya Times Fm ambapo alidai kuwa hivi sasa anafanya usajili wa wasanii wanaotaka kuingia kwenye hiyo label yake lenye lengo la kuwasaidia wasanii mbalimbali.
Alisema kuwa  hiyo itakuwa recording label ya kujitegemea itakayojikita katika kuwasaidia wasanii na kwamba yeye ni mmoja wa mdau  wa label hiyo.

“Ni Brainstorm Music, basically ni recording label ya kujitegemea ambayo itakuwa inasimamia kazi za wasanii nikiwemo mimi mwenyewe niko kwenye hiyo label. Ni kama recording label nyingine za nje ambazo unazisikika sijui Young Money, MMG, Cash Money, Bad Boys kwa hiyo it’s the same thing.” Amesema CPwaa.

“Nimeanzisha label yangu ambayo mimi niko chini yake pamoja na wasanii wengi tu ambao wamekuwa wakinifuata, wakiomba ushauri wakiomba miongozo na misaada ya kifedha. Kwa hiyo wote tutakuwa chini ya uongozi mmoja na shughuli zetu za kisanaa zitakuwa zinashughulikiwa na hiyo label.”

0 Response to "C PWAA AFUNGUA RECORDING LABEL YAKE "

Post a Comment