BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limedai kuwa kujitoa kwa wasanii
kushiriki Tuzo za Tanzania Kilimanjaro Muziki ni dalili za kuonesha uoga
wa kushindana na kutokubali kushindwa, huku ikiwataka mapromota
wajitokeze kuandaa tuzo nyingine zikiwemo ili kuibua ushindani.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Matukio Basata Meregesi Ng'oko, alipokua
akielezea historia ya tuzo katika kituo cha Star Tv jijini Dar es
Salaam, ambapo alisema kuwa kujitoa kwa baadhi ya wasanii kuwania tuzo
ni dalili kuwa wasanii hao wanaogopa kushindana na vipaji vipya
vinavyojitokeza.
Alisema kuwa BASATA wamepokea barua mbili rasimi za baadhi ya wasanii
waliojitoa kwenye tuzo hizo ambapo, ni msanii wa muziki wa kizazi kipya
nchini Dully Sykes, pamoja na bendiya Extra Bongo.
Baada ya kupokea barua hizo za kujiondoa kwa wasanii hao kwenye tuzo
BASATA, walifanya utafiti ili kujua nini sababu ya wasanii hao kujiondoa
katika tuzo hizo ambapo walibaini kuwa wengi hawapendi kushindanishwa.
"Unajua msanii baada ya kuona kundi alilopangiwa hatoweza kushindana
nalo ndipo inapokuja hiyo inshu ya kujitoa tena wengine bila hata ya
kuandika barua hiyo ni kwa sababu anaogopa kushindwa" alisema Ng'oko.
Vile vile alidai kuwa mapromota wajitokeze kwa wingi kuandaa tuzo
nyingine ili kuibua changamoto mbalimbali zitakazosababisha wasanii
kupokea tuzo nyingi tofauti tofauti.
Kwa upande wake Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa
tuzo za mwaka huu zimeboreshwa huku zikitoa fursa kwa wananchi
kuwapigia kura wasanii wanaowataka kuwania tuzo hizo.
Alisema kuwa bado wanaendelea kukumbwa na changamoto nyingi, huku
wakiendelea kuzifanyia kazi ili kureta mabadiliko ya tuzo hizo zionekane
bado zinatija. Alitoa mapendekezo kuwa kuwe na tuzo ndogo ndogo ili
kuboresha uchaguzi wa tuzo hizo.
0 Response to "BASATA - 'KUJITOA KWA WASANII KUOGOPA USHINDANI'"
Post a Comment