Latest Updates

Arnold Schwarzenegger kuanza kushuti toleo jipya la 'Terminator', kucheza kama Cyborg.

 Arnold Schwarzenegger kuanza kushuti toleo jipya la Mtunisha misuli na mkali wa filamu za kibabe na za kivita, Arnold Schwarzenegger ameeleza kuwa ataanza kushuti toleo jipya la filamu ya Terminator aliyoipa jina la ‘Terminator: Genesis’ mwezi April.
Arlnold ambaye aliwahi kuwa Governor wa California ameeleza kuwa itawachukua miezi minne hadi minne na nusu kushuti filamu hiyo na kwamba maeneo yatakayotumika ni New Orleans, San Francisco na huenda kidogo Los Angeles, na atacheza kama Cyborg.
“Toleo la mwishoni la Terminator ni wakati ambapo nilikuwa Governor kwa hiyo sikuwa katika filamu hiyo, lakini sasa nimerudi tena na kuna vitu vizuri kutokana na mimi kuwa kwenye filamu hiyo.” Alisema Arnold Schwarzenegger.

0 Response to " Arnold Schwarzenegger kuanza kushuti toleo jipya la 'Terminator', kucheza kama Cyborg."

Post a Comment