Msemaji
wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema kuwa rapper Lord Eyez
amesimishwa kazi katika kampuni hiyo na kwamba kwa sasa sio ‘member’.
“Kitu
ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha
kazi kikampuni.” Amesema Nikki wa Pili na kusisitiza kuwa hajafukuzwa
kazi bali amesimamishwa.
Hata hivyo, Nikki wa Pili hakuwa tayari kuweka wazi moja kwa moja sababu zilizopelekea Weusi kumsimamisha kazi rapper huyo.
“Hizo
ni confidential, ni issue za kampuni hatuwezi kuziweka wazi lakini Lord
Eyez tumemsimamisha kazi hiyo ndio taarifa ambayo tunaitoa kwa media.”
Nikki wa Pili ameeleza.
Ameongeza
kuwa kwa sasa matukio yote yanayotokea kwa upande wa Lord Eyez yatakuwa
yanamhusu yeye binafsi na hayatakuwa na uhusiano wowote na kampuni.
Hii inamaanisha hivi sasa Weusi inaundwa na Joh Makini, Nikki wa Pili, G-Nako na Bonta.
Uamuzi
huo wa Weusi umekuja wakati ambapo kumekuwa na taarifa kuwa Lord Eyez
alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi Jumamosi, huko Arusha
na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa
anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya 'Dell'.
Mwaka
juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi
wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe
msanii huyo.
Weusi
walichukua dhamana ya kumtetea na kumuwekea mwanasheria huku wakifanya
mikutano na waandishi wa habari ili kuitengeneza image ya kampuni hiyo
ambayo ilikuwa imewekewa alama na tuhuma za Lord Eyez ambaye ni member
wa kundi la Nako 2 Nako.
0 Response to "Nikki wa Pili asema 'Weusi' imemsimamisha kazi Lord Eyez"
Post a Comment