Latest Updates

AHUKUMIWA MIAKA 11 KWA KUMTAPELI JUSTIN BIEBER


MTU mmoja ambaye ni raia wa nchini Norway, Wahleed Ahmed, amejikuta akiwa maarufu kwa ajili ya utapele alioufanya kwa msanii Justin Bieber huko Scandinavia mwaka 2012.
Mtu huyo ambaye amefanya utapeli kiasi cha dola milioni 1 kwa mwekezaji kwa ajili ya ziara ya msanii huyo huko Scandinavia mwaka 2012 hali iliyopelekea kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo za utapeli.
Wahleed alijikuta akipatikana na tuhuma hizo za utapeli hali iliyosababisha kuwa maarufu ambapo amepatwa na hatia hiyo hali iliyopelekea kuhukumiwa kifungo cha miaka 11 jela.
Mbali na kutumikia kifungo hicho, ametakiwa pia kurudisha kiasi hicho cha fedha alichotapeliwa ambapo iligundulika kuwa alitumia nyaraka feki pamoja na tovuti alizonunua mtandaoni akijifanya mfanyabisahra mkubwa ili kufanikisha uhalifu wake.
Jaji Philip Gutierrez ambaye ndiye alikuwa anasikiliza kesi hiyo, ameamuru pia kwa mtuhumiwa huyo kuwa chini ya uangalizi kwa miaka mingine mitatu baada ya kumaliza kifungo chake hali hiyo imetokana na rekodi ya matukio yake mengi makubwa ya utapeli.

0 Response to "AHUKUMIWA MIAKA 11 KWA KUMTAPELI JUSTIN BIEBER "

Post a Comment