MSANII wa miondoko ya Hip Hop kutoka nchini Marekani Rick Ross ameamua
kubadilisha mfumo wake wa maisha ili kuzuia matatizo mbalimbali yakiwemo
kuugua, pamoja na kuboresha afya yake.
Rapper huyo amebadilisha mfumo wake wa kula na jinsi anavyoishi ili
kuupa mwili wake afya njema na kujizuia na magonjwa yakiwemo ugonjwa wa
moyo.
Miaka miwili iyopita ilishawahi kuripotiwa kuwa rapper huyo alishawahi
kupoteza fahamu akiwa kwenye ndege akielekea Florida hali iliyopelekea
kusabababisha ndege hiyo kutua ili apatiwe huduma.
Alifanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa uzito wa mwili wake na kukosa usingizi wa kutosha ndio ulisababisha hali hiyo.
Baada ya hali hiyo ameamua kubadili mfumo mzima wa maisha yake ambapo
anafanya mazoezi mara mbili kwa siku, huku akila chakula kwa ajili ya
afya na kupata muda wa kupumzika.
Pamoja na hayo alifanya maojiano na kutangaza ujio wake wa albamu yake mpya .
0 Response to "BAADA YA KUGUNDUA UZITO WAKE UMEONGEZEKA, RICK ROSS ABADILI MFUMO WA MAISHA "
Post a Comment