Latest Updates

WASANII 12 WATINGA BIUNGE LA KATIBA


                                        John Kitime, Simon Mwakifwamba
Wasanii 12 wakiwemo viongozi toka Shirikisho la muziki, Shirikisho la Filamu, Shirikisho la Sanaa za ufundi, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania walifunga safari na kuvamia Dododma na kuwa na mfululizo wa mikutano na wabunge mbalimbali ili kuwashawishi waunge mkono vipengele viwili ambavyo wasanii wanavitaka katika Katiba
                                 Joseph mbilinyi,John Mnyika, John kitime, simon mwakifwamba
wasanii kutambuliwa katika Katiba kama vile walivyotambuliwa Wakulima, wafugaji, wavuvi na wafugaji walivyotajwa

Milliki Bunifu kwa kiingereza Intellectual Property ambamo ndani yake kuna Hakimiliki itajwe rasmi katika Katiba hili litawezesha sheria mwafaka zitungwe katika kuendeleza sanaa na kulinda kazi za sanaa na kazi za ubunifu. Kundi hili limepokelewa vizuri sana na wabunge wote lililokutana nao.
                                                    Simon Mwakifwamba, Yvonne chellyl, kitime
Ni hatua nzuri na historia inajengeka kwa mara ya kwanza katika kupigania tasnia kutambulika kwa maslahi na kutoa ajira kwa jamii kubwa huku ikiwa ni sehemu ya kujenga uchumi usiotegemea madini na vitu vingine, endapo burudani itatambuliwa na kuingia kuwa sekta rasmi tatizo la ajira litapungua kwa asilimia kubwa.

0 Response to " WASANII 12 WATINGA BIUNGE LA KATIBA "

Post a Comment