MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Roma Mkatoliki atangaza ujio
mpya wa nyimbo yake ambayo itakujua na utaratibu mpya aliojiwekea kwa
kutoa single zaidi ya moja kwa mwaka mzima.
Roma ambaye amekuwa na kawaida ya kutoa single moja kwa mwaka mzima hivi
sasa hali itakuwa ya tofauti ambapo amedai kutoa nyimbo zaidi ya moja
kwa muda wa mwaka mzima.
Akizungumza na jarida hili Roma alidai kuwa mwaka huu atakuwa na
utaratibu wa tofauti kwa kutoa nyimbo zaidi ya moja hiyo ni kutokana na
ushauri wa mashabiki wake.
"Nitakuwa natoa nyimbo tatu kwa mwaka mmoja huu ni utaratibu mpya ambao
mashabiki zangu wameshauri hivyo na mimi nafanya kazi kwa sababu ya
mashabiki hivyo ndio maana nimefwata walichokuwa wakitaka" alisema Roma.
Alisema kuwa hivi sasa kutakuwa na tofauti kubwa ya ufanyaji wake wa
kazi hii ni kutokana na mazingira ya muziki kubadilika kutokana na
nyimbo nyingi kurekodiwa kila siku.
0 Response to " ROMA AJA KIVINGINE"
Post a Comment