Latest Updates

MUIGIZAJI AFARIKI DUNIA


                        

MUIGIZAJI amaarufu nchini Marekani Seymour Hoffman amefariki jana usiku nyumbani kwake huko New York Marekani ambapo inadaiwa kuwa sababu ya kifo chake ni matumizi ya dawa za kulevya.

Muigizaji huyo ambaye pia alikuwa mshindi wa tuzo za Oscar inasemekana kuwa alifiikwa na umauti huo nyumbani kwake .


Vyanzo vya habari vilieleza kuwa Hoffman amekutwa bafuni kwake akiwa amevaa bukta huku mkononi kwake akiwa ameshikilia sindano inayosemekana alikuwa akiitumia kwenye matumizi hayo ya dawa za kulevya.

                  
Inadaiwa kuwa polisi walikuta bahasha 10 zilikuwa dawa aina ya heroin na zingine tupu, ambapo inadaiwa kuwa alizidisha utumiaji wa dawa hizo.

Askari wanasema Hoffman alitakiwa kuwapitia watoto wake jumapili asubuhi mida ya saa tatu ilivyofika muda na baba yao hakutokea ndipo ndugu wkajua kuna tatizo ukizingatia sio kawaida yake.

0 Response to "MUIGIZAJI AFARIKI DUNIA"

Post a Comment