IKIWA kila ifikapo Februari 14 ni siku ya wapendanao duniani, utafiti
uliofanywa na shirika la Ipsos, lenye lengo la kujua ni nchi gani ya
Afrika Mashariki inayoongoza kwa kuilewa siku hiyo ya wapendanao.
Utafiti huo ulilenga watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika miji
mikubwa ya nchi tatu Kenya, Uganda pamoja na Tanzania ili kujua uelewa
kuhusu suala zima la siku ya Mtakatifu Valentine.
Waliohojiwa ni jumla ya watu 528 kutoka Tanzania, 1050 Kenya na Wangana
1006, ambapo utafiti huo ulizingatia jinsia, wanawake na wanaume,
mahojiano hayo yalifanywa kwa kutumia msaada wa computer na simu.
Katika nchi hizo tatu utafiti ulifanywa tarehe 7 hadi 10 mwezi februari 2014
Katika utafiti huo umebaini kuwa Tanzania kwa ujumla wake na nia ya siku
hiyo wanaume ndio wanania ya kusherehekea zaidi siku hiyo kuliko
wanawake
Kwa mujibu wa tafiti hizo kwa nchi hizo tatu tanzania imepata asilimia
72 inayoamini kuwa siku hii itakuwa ya mashamsham ya mapenzi zaidi
kuliko nchi nyingine ambapo Uganda imepata asilimia 56, kenya
inaasilimia 52.
Inadaiwa pia siku hii ya wapendanao, matumizi yanabadilika ambapo
wataznania wamepata asilimia 42, kutegemea kununua nguo kuliko vitu
vingine wakati Uganda inaasilimia 37, pamoja na Kenya asilimia 36
kununua maua zaidi.
0 Response to "KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WATANZANIA WAONGOZA KUSHEREHEKEA SIKU YA WAPENDANAO,"
Post a Comment