Latest Updates

BASATA YAZIDI KUMWEKEA NGUMU SNURA
                               
Snura Mushi mwigizaji wa filamu ambaye anafanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya amesikitishwa na kitendo cha video ya wimbo wake wa Nimevurugwa kufungiwa kuonyeshwa katika vituo vya televisheni na Basata eti kwa sababu ya imekosa maadili.
Video ya kawaida kabisa na nimecheza mwenyewe na wacheza show wangu, na nilifanya hivyo baada ya video yangu ya Majanga kulalamikiwa kuwa sikucheza,”
“Ni tatizo inakatisha tamaa wasanii wa Tanzania ndio tunaangaliwa lakini video za nje zipo na picha mbaya lakini hatujasikia zimefungiwa,”anasema Snura

Snura ambaye nyota yake inang’ara katika filamu na muziki anasema kuwa pamoja Serikali kujaribu kuangalia suala la ajira kwa vijana lakini changamoto ni nyingi sana wanazopambana nazo hasa suala la ushindani na kazi kutoka nje ambazo haziangaliwi na kupigwa marufu kuchezwa kama kazi za wasanii wa nyumbani.

0 Response to "BASATA YAZIDI KUMWEKEA NGUMU SNURA"

Post a Comment