Latest Updates

GAVIN PASLOWONE ANUNUA USHETANIMWANAUME mwenye umri wa miaka 43, anayejulikana kwa jina la Gavin Paslowone anayeishi Kent nchini Uingereza ameamua kutumia zaidi ya pauni 10,000 ili kujibadilisha sura ili afananae na shetani anayeishi.
Mwanaume huyo ambaye anawatoto wawili ameachana na mkewe wake anasema mabadiliko hayo ni magumu na yenye gharama kubwa alianza kufanya mwaka 2007.
Ambapo hadi sasa ameshakata ulimi wake ili kuwa na ndimi mbili, kabadilisha meno yake kuwa na ncha kali kujiweka mapembe kwenye paji la uso wake.
Inadaiwa kuwa hivi sasa anamikakati ya kuweka nati katika fuvu la kichwa chake ili aonekane kuwa na manundu na ming'ao ya kishetani.
Mwanaume huyo amechonga masikio yake kuwa na ncha na kuchora tatto kwenye sura yake na mikono kufanana kwake na shetani hali iliyompelekea kuwa ngumu kupata msichana wa kuishi naye tena.
"Nilichagua kuwa shetani mtu kwani kila kitu kimeshafanyika hapa duniani mi si shetani na wala sina mawazo hayo ni furaha tu ya moyo wangu, napenda ninavyoonekana haswa ninachohitaji kwa sasa ni mkia na sio mkia wa bandia mkia halisi wenye kuishi" alisema.

0 Response to "GAVIN PASLOWONE ANUNUA USHETANI"

Post a Comment