Latest Updates

SNURA AWAPA UKWELI MAPROMOTA WAZULUMATI MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mcheza filamu nchini, Snura Mushi amesema alishawahi kudhulumiwa na baadhi ya mapromoto, ambao wanaandaa shoo mbalimbali nchini. 

Akizungumza na jarida hili msanii huyo, alisema kuwa bado kazi ya muziki ina misukosuko na kuhitaji uvumilivu kwa upande wa baadhi ya mapromota kwani wanawalipa kiasi kidogo cha fedha na wengine kuwadhulumu. 

Kutokana na baadhi ya mapromota kushindwa kuwalipa fedha halali inayoendana na kazi aliyoifanya, hali hiyo inasababisha baadhi ya wasanii kuendelea kuishi maisha ya kawaida tofauti na kazi wanayoifanya. 

Alisema alishawahi kudhurumiwa na baadhi ya mapromota zaidi ya mara mbili, wakati tayari alishamaliza kufanya shoo alizoandaliwa. 

"Mimi nimeshawahi kudhulumiwa zaidi ya mara mbili, lakini sasa nitafanyaje, bado kuna tatizo kwa baadhi ya waandaaji wa shoo za muziki ambao wanatoa malipo tofauti na kazi msanii uliyoifanya," alisema Snura. 

Pamoja na hayo msanii huyo anatarajia kutoa wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la 'Ushaharibu' ambao ndipo utakuwa zawadi kwa mashabiki wake mwaka huu. Alisema kama kawaida yake ya kuigusa jamii, katika tungo zake ndicho alichokifanya kwenye wimbo huo ambao ameigusa jamii kwa tungo zinazoishi na maisha yao ya kila siku. 

0 Response to "SNURA AWAPA UKWELI MAPROMOTA WAZULUMATI"

Post a Comment