Latest Updates

SHILOLE KWENDA MAREKANI
MSANII wa muziki nchini Zuwena Mohamed 'Shilole' anatarajia kwenda nchini Marekani kwa ajili ya safari ya kimuziki mwanzoni mwa mwezi wa pili, hii ni miongoni mwa safari zake za kujinadi kwa kazi ya muziki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Shilole alisema kuwa ziara za kikazi za kimuziki nje ya nchi zinamjenga na kumuongezea mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa anatarajia kwenda Marekani katikati ya mwezi wa pili ikiwa ni moja wapo ya ziara zake za kimuziki ambapo mwishoni mwa mwaka alikuwa nchini Uingereza.

Pamoja na hayo msanii huyo amedai kuwa kufanya shoo nje ya nchi ni moja ya mafanikio ambayo alikuwa akiyategemea kila siku katika kazi zake, hivyo anaamini shoo hizo zinamjenga na kumpa uwezo.

Anatarajia kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la 'Chuna Buzi' ambayo ndio ujio wake mpya kwa mwaka huu, huku akitarajia kufanya shoo Jumapili akishirikiana na Mzee Yusuph.

0 Response to "SHILOLE KWENDA MAREKANI"

Post a Comment