Latest Updates

MCD WA TWANGA PEPETA KUZIKWA LEO

ALIYEKUWA mpiga tumba wa bendi ya muziki wa dansi, The African Stars 'Twanga Pepeta' Soud Mohamed 'MCD' amefariki juzi usiku katika hospitali ya KCMC mjini Moshi, ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

MCD alipelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya kifua kikuu kilichokuwa kikimsumbua kwa muda mrefu

Akizungumza na jarida hili jana kwa simu kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu alisema mwanamuziki huyo anatarajiwa kuzikwa leo mjini Moshi, ambako ndiyo nyumbani kwao.

Luiza alisema walitarajia kukutana jana na wadau wa bendi hiyo kwa ajili ya kupanga safari ya kwenda Moshi na kulikuwa na uwezakano mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki wangeondoka jana usiku kwa ajili ya kuwahi kuzika.

MCD pia wakati wa uhai wake, aliwahi kuzitumikia bendi nyingine za Diamond Sound na Mashujaa Musica.

0 Response to "MCD WA TWANGA PEPETA KUZIKWA LEO"

Post a Comment