Latest Updates

DJ KUINGIA ANGA ZA JUU AFRIKA


DJ mmoja mwenye umri wa miaka 25 nchini Afrika Kusini anatarajiwa kuwa mwafrika wa kwanza kufika katika anga ya juu zaidi. Mandla Maseko ni mmoja wa watu 23 ambao wamejishindia nafasi ya kuweza kufika katika anga ya juu mnamo mwaka 2015.

''Anga sasa inafikika-ilikuwa ni kama ndoto ya mbali kwa watu kama mimi.Sasa hivi inawezekana na natumai watu watazidi kujihusisha nayo.Anafafanua alivyowashinda watu milioni moja kutuzwa nafasi hiyo. Nilitaka kufanya jambo lisilo la kawaida-Napenda kujaribu mambo mapya na hii ilikuwa fursa nzuri kwangu.

Mwanzoni niliona tangazo la kibiashara la shindano hilo kwenye runinga na baadaye kwenye redio.Nilihitajika kutuma picha yangu nikiruka kutoka popote pale.Hivyo basi nikaruka kutoka ukuta mrefu na rafiki yangu akanipiga picha nusu hewani.

Nilitakikana pia kujibu maswali na kueleza kwa nini nilitaka kutalii anga ya juu.Jibu langu lilikuwa;’Nataka kuvunja sheria za uzito na kuandikwa kwenye vitabu vya historia kama mwafrika wa kwanza kutua angani’

Nilikuwa mmoja wa watu thelathini waliochaguliwa kuenda katika kambi ya anga iliyoko Parys,Free State.Nilihitajika kupitia majaribio matatu-mawili yakiwa ya lazima.Moja ilikuwa kuruka kutoka futi 10,000 hadi kwenye ardhi na nyingine ilikuwa ni tapiko la nyota wa mkia.

0 Response to "DJ KUINGIA ANGA ZA JUU AFRIKA"

Post a Comment