Latest Updates

ROSE NDAUKA AMFICHA MTOTO WAKE

Baada ya kujifungua mtoto wa kike msanii wa filamu nchini Rose Ndauka adai kuwa hana mpango wa kuiweka picha ya mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii kwa kipindi hichi hadi hapo watakapoamua.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Ndauka aliweka wazi kuwa bado ajafikiria kuweka picha yoyote ile kwenye mitandao ya kijamii hadi hapo muda utakapofika, hali hiyo inaonesha kuwa picha ya mtoto wake huyo kuwa adimu kwenye mitandao ya kijamii tofauti na ilivyozoeleka kwa baadhi ya watu.

"Bado sijafikiria kuweka picha yoyote sasa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu bado mwanangu hajafikia hatua hiyo, na muda ukiwa teyari nitaiweka mwenyewe hivyo mashabiki wangu watapata nafasi ya kumuona hapo kwa mara ya kwanza" alisema Ndauka.

0 Response to "ROSE NDAUKA AMFICHA MTOTO WAKE "

Post a Comment