Latest Updates

NISHA ADAIWA KUCHOROPOA MIMBA

nisha rr 538
Nyota wa filamu Tanzania, Salma Jabu maarufu kama Nisha yamemkuta makubwa baada ya habari kuvuja kuwa kumbe sababu ya kuumwa hadi kuzidiwa kitandani, ilitoka na kuchoropoa mimba changa aliyokuwa nayo.
Mtu wa karibu wa msanii huyo ambaye yupo ndani ya familia hiyo baada ya kusambaa kwa habari kuwa Nisha aliugua gonjwa la ajabu ghafla katika mitandao ya kijamii

Wakati awali ikidaiwa kuwa msanii huyo alikumbwa na maumivu ya kichwa pamoja na kuona maluweluwe, lakini imebainika kwamba kilichosababisha ni kitendo chake kisicho cha kimaadili cha kuitoa mimba, bila kujua kuwa baadhi ya wanawake wenzake huzitafuta kwa udi na uvumba.

nishai 536
baada ya kupigiwa simu alisikika akisema

“Jamani huo uzushi tu toka kwa watu wasionitakia mema, kama kweli nilitoa mimba, kwa nini nilikuwa naumwa na kichwa na binadamu siyo wazuri, mbona wao wanafanya mambo yao hakuna mtu wa kuwafuatilia, jamani watu tuishije mbona majanga?” alijieleza msanii huyo baada ya mapaparazi wetu kufika nyumbani kwake.

Hata hivyo, Nisha alimshutuma mmoja wa wasanii wa kike wa Bongo movie (jina linahifadhiwa) akimtaja kuwa ndiye anayemfuatilia maisha yake kwa kumpakazia ishu hiyo, akidai itatokana na wivu wa maendeleo yake.

0 Response to "NISHA ADAIWA KUCHOROPOA MIMBA "

Post a Comment