Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuachana urafiki na
meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha
mafanikio nyuma yake yupo Kadinda jambo anasema hana rafiki aliye wa
karibu kuliko meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vyema.“Kadinda
ndiye kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda
mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho
tuliyoachana hivyo inakuwa kama sijapoteana naye ni kama vile nipo naye
kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.

Msanii
huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless Fame film
alifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri kwa hadhi yake
anastahili kuwa na kampuni na kuachana kuigiza filamu za watu wengine.
0 Response to " WEMA AMWAGIA SIFA MENEJA WAKE"
Post a Comment