Latest Updates

'KIBABABABA' YABADILISHA MTINDO WA KUNDI LA MAKAMANDOWasanii wa muziki wa bongo fleva wanaounda kundi la Makomando Fred Felix 'Fred Wayne', pamoja na Said Christopher 'Mucky' wamedai kuwa nyimbo yao mpya inayokwenda kwa mtindo wa 'kibabababa' imebadilisha mfumo wa maisha yao pamoja na kuwaongezea mashabiki lukuki.

Akizungumza na jarida hili Fred Wayne amedai kuwa nyimbo hiyo imepokelewa vyema na mashabiki hali iliyopelekea kupata shoo nyingi kwa kipindi hiki cha mwezi huu wa kwanza ingawa ni mwezi mgumu kufanya shoo.

Kutokana na hilo amesema kuwa kundi hilo limezidi kung'aa kwa kufanya shoo nyingi kwa mwezi huu, huku wakiendelea kupokea mialiko ya kufanya shoo mbalimbali kwa kipindi cha miezi 5 mfululizo.

Ameeleza kuwa kuendelea kupata shoo nyingi hizo ni kutokana na nyimbo yao hiyo kuendelea kufanya vizuri ambapo nyimbo hiyo sasa inamwezi tangu imeachiwa lakini imeonekana kufanya vizuri.

"Hii nyimbo ya mtindo wa kibababa imetubadilisha vitu vingi kwenye soko la muziki sasa nyimbo yetu inatuuza kwa kipindi hiki tumeona mabadiliko mwengi na bado inaendelea kiufanya vizuri" alisema Fred.

Alieleza kuwa siri ya kufanikiwa kwenye muziki ni kuwa mbunifu hususani katika kutunga mashairi na kutengeneza video yenye ubora huku mtayarishaji wa muziki kuendelea kuwa mbunifu katika kuchanganya vyombo.

0 Response to "'KIBABABABA' YABADILISHA MTINDO WA KUNDI LA MAKAMANDO "

Post a Comment