Latest Updates

CCM NA CHADEMA WAZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KIBORILONI

SAM_0309Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita (Kushoto)
akiteta jambo na Mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Kibor0loni kwa
tiketi ya chama cha Mapinduzi, Willy Adriano, wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo kuziba pengo lililoachwa wazi na
aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata hiyo,, Marehemu Vincent Rimoy
aliyefariki dunia Novemba 6, mwaka jana.

SAM_0314Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanajro, Iddi Juma,
(aliyeshika kipaza sauti), akimnadi mgombea wa CCm katika Uchaguzi
mdogo wa Udiwani, Wlly Adriano katika uchaguzi uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo
lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwanbi wa Kata ya
Kiborloni, Vincent Rimoy, alyefariki dunia ghafla Novemba 6 mwaka
jana.
SAM_0318Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi (kushoto), akiwa
akimtambulisha Mgombea wa Udiwani katika kata ya Kiboriloni, Willy Adriano aliyesimama katikati, kulia kwake ni Mke wake.(Picha zote na Taifa Letu.com Blog)
…………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Moshi
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mwishoni mwa wiki walifanya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi
mdogo wa udiwani katika kata ya Kiboriloni liliachwa wazi kufuatia
kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Vincent Rimoy (CHADEMA), aliyefariki ghafla Novemba 6 mwaka jana.
Wa kwanza kufanya uzinduzi ni Chadema, waliozindua kampeni yao kwa mbwembwe wakimtambulisha mgombea wao, Frank Kagoma ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi, uzinduzi ulioongozwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani hapa akiwemo mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemon Ndesamburo.
Wakizungumza katika Nyakati tofauti katika uzinduzi huo uliofanyika, Jumamosi ya Januari 18, mwaka huu, katika stendi ya kidia, viongozi wa Chadema walianza kumnadi mgombea wao ambap[o walimtaja kama mtu sahihi ambaye anaweza kuendeleza mapambano ya chama hicho ndani ya baraza la madiwani kupinga ufisadi na uonevu katika manispaa ya Moshi.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, aliwataka wananchi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa Chadema kwani ndiye mwenye uwezo wa kutekeleza yale yote aliyoyaanzisha Marehemu Rimoy ndani ya kata hiyo na baraza la madiwani.
“Wananchi wa kiboriloni msidanganyike, chaguo la kweli katika maendeleo ya kata hii ni Kagoma, katika kipindi chake kama mwenyekiti Kagoma alifanikiwa kuvunja magenge yote ya ujambazi na sasa mnatembea
vifua mbele bia wasiwasi, tupeni kagoma tuendeleze moto wa Chadema ndani ya Baraza la Madiwani, tupeni kagoma tukamalizie kazi aliyoianzisha Rimoy,” alisema Rimoy.
Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemona Ndesamburo alisema kazi ya kuleta maendeleo katika kata hiyo na mkoa kwa ujumla unaweza kufanywa na watu makini wenye uthubutu kama alivyo na uthubutu Mgombe wa kiti hicho, Frank Kagoma.
Kwa upande wao, Chama cha Mapinduzi CCM, waliofanya uzinduzi wao juzi, kwa kumtambulisha mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Wlly Adriano walisema Maendeleo ya kata ya Kiborloni ni zaidi ya itikadi za siasa na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya uamuzi sahihi.
Akizungumza na maelefu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya stendi ya Kidia, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi alisema wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitafuta madaraka kwa njia mbalimbali, ikiwemo kufanya vurugu na maandamano.
“Unajua ukisikia nchi fulani ina maendeleo kiuchumi, kisiasa na mambo mengine ni kwa sababu kuna amani, kwa hiyo hili jambo ndugu zangu ni muhimu sana kulizingatia ili kutuwezesha kuendelea na kazi zetu za kijamii vizuri” alisema Kazidi.
Kwa upande wake Mchumi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, aliwataka vijana kutokuuza shada zao za kupigia kura kwani kufanya hivyo ni kuuuza maendeleo yake.
Aidha Matemu aliongeza kwa kusema kuwa siasa bila maendeleo hakuna kujenga msingi wa kuleta maendeleo, na kuwataka wananchi wa kata ya kiboriloni kuchagua Willy Adriano ili aweze kuwawakilisha katika baraza la madiwa la Manispaa ya Moshi.
Naye Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano, alisema Siasa za Tanzania haziwezi kupiga hatua endapo wananchi hawatabadilika na kuacha tabia ya kuchaguana kwa kuangalia kigezo cha itikadi za kisiasa.
Uchaguzi mdogo wa udiiwani katika kata ya Kiboriloni uunarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi

0 Response to "CCM NA CHADEMA WAZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KIBORILONI "

Post a Comment