Latest Updates

MSANII WA KENYA JAGUAR ATUMIKIA KIFUNGO
Msanii kutoka nchini Kenya anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo,  Kigeugeu na kipepeo Jaguar yupo mbioni kutoa wimbo wake mpya wa “Kioo” ambayo nyimbo hiyo inazungumzia maisha ya ujana.
Katika nyimbo hiyo ameamua kuonesha kitu cha tofauti ambapo maudhui ya wimbo huo unazungumzia hasa ujana na matatizo tofauti na jinsi unavyo weza kujifunza kutoka kwenye mambo mazuri na mabaya unayofanya.Ili kuonesha kitu cha kipekee msanii huyo imemlazimisha Jaguar kuingia jera kama mfungwa nchini Kenya ili aweze kuiboresha video hiyo.
Baadhi ya picha za utengenezwaji wa Picha za video zinamuonyesha Jaguar akiwa jela na wafungwa huko Kenya. Jela hii ya Industrial Area imeruhusu J Kufanya baadhi ya vipande vya video yake humo akiwa na wafungwa wa gereza hilo

0 Response to " MSANII WA KENYA JAGUAR ATUMIKIA KIFUNGO "

Post a Comment