Latest Updates

JOKETI AFUNGUA CLUB YAKE


MBUNIFU wa mitindo ya nguo na nywele aina ya 'Kidoti brand' Jokate Mwegelo afungua club yake ijulikanayo kama Kidoto club.

Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Jokate alisema kuwa Kidoti klub ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii husani masuala ya urembo na mitindo.

Jokate alisema kuwa lengo lake kubwa la kuanzisha club hiyo ya Kidoti ni kusaidia jamii pamoja na kupanua mtandao wake hivyo anaamini watu wengi watajiunga naye.

Aliweka wazi kuwa kupitia club yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti.

Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 alisema ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno  kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ngíaringíari.

ìHuu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii, Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu atakayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,î alisema Jokate

Jokate aliongeza kuwa kupitia Klub hiyo atakuwa akiandaa na kuendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.
                                                  
                                                    by Zourha Malisa

0 Response to "JOKETI AFUNGUA CLUB YAKE "

Post a Comment