Latest Updates

ROMA PROFILEJina Kamili :   Ibrahim Mussa
Jina la kisanii :  Roma Mkatoliki
Msanii wa miondoko : Roma ni msanii mkali wa Hip Hop Tanzania, ambaye tangu aanze kazi yake ya muziki amekuwa akiimba miondoko hiyo ya Hip Hop.
Alianza safari ya muziki lini ? : Safari yake ya muziki alianza mnamo mwaka 2006 akiwa mkoani Tanga, ingawa inadaiwa kuwa alitoroka shule asubuhi ili aweze kuonana na mtangazaji maarufu B. Twelve ambaye alienda mkoani hapo kwa ajili ya shoo.
Lini aliingia studio ? :  Mwaka 2007 aliweza kurekodi nyimbo yake ambayo aliipa jina la 'Salute' ambayo alifanya studio ya Gomba Record.
Sigle yake ya kwanza alitoa lini ?:  Mnamo mwaka 2008 aliweza kufanikiwa kurekodi nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Tanzania' ambayo ndio miongoni mwa nyimbo ambayo imemtambulisha kwenye gemu la muziki nchini.
 Aliweza kuingia studio :  2007 niliweza kurecod ngoma ya kwanza iliyokuwa inajulikana kwa jina la SALUTE kwa producer abbuy .

Alifika Dar Lini ?: Mwaka 2008 ndio mwaka ambao nimeweza kufika dar rasmi kuishi na kuweza kurekodi TANZANIA .
Mbali na muziki anafanya nini? :  Mbali na kuwa msanii wa Hip Hop pia ni mchezaji mpira wa kikapu ambapo ameanza kucheza akiwa mdogo mtaani kwao ambapo alikuwa na timu ya mpira wa kikapu huku akiwa na ndoto ya kuwa mchezaji maarufu igawa ndoto hizo zimezimwa na muziki.
Alianza kucheza mpira wa kikapu lini?:  Roma alianza kucheza mchezo huo akiwa mdogo, huku akichezea timu yake ya mtaani akiwa anacheza namba 1,na 2 ingawa mwili wake unaonekana anaweza kucheza namba 5 kama 'big'.
Awa kocha:  Baada ya kuacha kucheza mchezo huo, ameweza kuendeleleza kipaji chake cha mchezo huo wa mpira wa kikapu ambapo ameweza kuwa kocha wa timu yake ya mtaani.

Sababu zilizosababisha awe kocha wa mpira wa kikapu : Kwa sasababu anapenda kuendelea kucheza mchezo huo wa mpira wa kikapu aliamua kujiunga kuwa kocha ili aweze kuendeleza kipaji chake.

Amejikita na masuala ya ujasiliamari : Mbali na kucheza mchezo huo pia ni mjasiriamali ambaye ameanza kufanya biashara mara baada ya kuanza kufanya muziki wake wa miondoko ya Hip Hop.
Mwanafunzi wa chuo:  Pamoja na hayo yeye ni mwanafunzi wa ngazi ya Stashahada  ambapo anampango wa kuendelea kujiendeleza na elimu ya chuo huku akidai kuwa elimu ni moja ya jambo ambalo anaamini ataliendeleza.
Ameshapokea tuzo ngapi?: Ameshawahi kupokea tuzo mbili za muziki wa Kilimanjaro, ameshapokea tuzo ya msanii bora wa Hip Hop kwa kupitia wimbo wake wa Mathematics, na wimbo bora wa Hip Hop. 
Kitu ambacho hawezi kukisahau?:  MWAKA 2006 akiwa tanga amewahi kutoroka shule asubuhi akamfwata B.TWELVE aliyekuja tanga nadhani kwenye show ya park lane, alifanikiwa kukutana naye kwenye gari na kumkabidhi cd zenye nyimbo mbili ambazo alimuomba azipige lakini hazikufanikiwa.
 
                                                      by Zourha Malisa

0 Response to " ROMA PROFILE"

Post a Comment