Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini anayeimba miondoko ya Hip Hop
Wakazi kesho anatarajia kuzindua video wa wimbo wake unaojulikana kwa
jina la 'Touch' ambayo aliitumbuiza kwa mara ya kwanza nchini Afrika
Kusini katika Big Brother The Chase.
Msanii huyo katika uboreshaji wa kazi yake hiyo ameamua kuvujisha wimbo
ambao hakuwa rasmi alioupa jina linalojulikana 'Wanawake wa Dar'.
Nyimbo hiyo ambayo inapatikana katika mixtape yake inayojulikana kwa
jina la 'I am Afrika Mixtape' inatarajia kutoka hivi karibuni.
Akielezea sababu za kuivujisha nyimbo hiyo ya wanawake wa Dar alieleza
kuwa anaamini kuwa itafanya vizuri huku nyimbo yake ya 'Touch' kuendelea
kufanya vizuri zaidi katika vituo vya radio kwa sasa.
0 Response to "WAKAZI KUZINDUA 'TOUCH' "
Post a Comment