Latest Updates

MSANII ALIE WAI KUIBIWA WIMBO WA FOLOW ME NA RICH MAVOCO APATA USIMAMIZI.

 
Msanii chipukizi anaechipukia jina lake kamili ni Adam Mustafa kwa jina la sanaa ni Chismo, alishawai kusikika na skendo ya kuibiwa wimbo wake na Rich Mavoco na kufanya vizuri “Folow me” ameingia mkataba na kampuni ya Machapta chini ya Machapta Inc kwaajili ya usimamizi wa muziki wake kwa miaka mitatu.
                              
Kwasasa Chismo amesha saini mkataba huo na yupo mbioni kukamilisha video yake ya kwanza kufanya katika kampuni hiyo jumapili hii na ameshaanza kurecord nyimbo katika studio tofauti tofauti za hapa nchini.

 
Kwa upande wake Chismo anafunguka na kusema nilianza mziki kama dansa na nilifanya kazi ya udansa kwa Bob Junior nikatoka nikaenda kwa Dully Sykes nandipo nikaamua kuungana na Baby J lakini ndoto yangu haiku kamilika na kunakipindi Tunda man alikua anafanya poa nikaamua kumuomba na akanikubalia kwakua alikua anaona uwezo wangu ila muda ulivyo zidi kwenda ndio nikakutana na Rich Mavoco na nikafanya nae pia kazi lakini nikiwa nae mazoezini Rich nilikua naimba nyimbo yangu ya Folow me na yeye alikua anaipenda sana na akawa ananirecod kumbe mwezangu akaingia stodio na kufanya kweli, Kote nilipo pita ilikua kama sehem yangu ya kujifunzia tu.Machapta Inc ni Lebo mpya iliyo zaliwa chini ya Machapta Production iliyopo kinondoni vijana...

0 Response to "MSANII ALIE WAI KUIBIWA WIMBO WA FOLOW ME NA RICH MAVOCO APATA USIMAMIZI. "

Post a Comment