Latest Updates

SHAA ATAMBA SUGUA GAGA KUVUNJA REKODIMSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Sarah Kaisi 'Shaa' ameweka wazi kuwa nyimbo yake aliyoitoa hivi karibuni inayojulikana kwa jina la 'Sugua Gaga' imevunja rekodi kwa kuangaliwa na watu zaidi ya elfu 20,000 kwa muda wa siku tatu.
Akizungumza na mwandishi wa habari  hili msanii huyo aliweka wazi kuwa nyimbo hiyo imevunja rekodi ambayo haijawahi kutokea katika kazi zake za muziki hali ambayo inampa nguvu ya kuona mashabiki wanafwatiria kazi zake na kuzikubali.
Akielezea sababu ya wimbo huo kuvunja rekodi hiyo Shaa aliweka wazi kuwa ubunifu wa video hiyo na jisni alivyoimba ndio sababu pekee ilionesha ubora wa kazi hiyo.
Alisema kuwa ni mmoja kati ya wasanii wanaopokea mabadiliko na kuimba kutokana na mazingira yoyote anayokutana nayo hali inayompa uzoefu na kumjenga kwenye kazi yake hiyo ya muziki.
Akielezea wazo la wimbo huo alidai kuwa ni wimbo huo amekuta teyari umeshatungwa na ilikuwa wazo la   Saidi Fella ambapo aliyekusudiwa kuimba alikuwa ni kijana wa kiume lakini kutokana na uwezo wake aliweza kuumudu wimbo huo na kuufanya kuwa wake.
"Mimi wimbo nilikuta teyari umeshatungwa kila kitu na alitakiwa kuimba mwanaume lakini mimi nikapewa ilinichukua siku mbili kuufanyia mazoezi na kuumudu wimbo huyo" alisema Shaa.
Nyimbo hiyo ya 'Sugua Gaga' imetengenezwa chini ya udhamni wa Mkubwa na Wanawe.

1 Response to " SHAA ATAMBA SUGUA GAGA KUVUNJA REKODI"