LULU ALONGA NA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Elizabeth Michael ‘Lulu’ambae ni msanii wa filamu Nchini, ameliomba Bunge kurekebisha sheria za Magereza katika vikao vyao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Lulu alisema kutokana na kukaa huko kwa mwaka mmoja, ameona mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.
“Unaweza ukamkuta mfungwa ana miaka zaidi ya 20 lakini hajawahi kufikishwa mahakamani wala kuulizwa chochote kutokana na kitu ambacho kimempeleka hapo, kiukweli hata kama ana makosa haiwezekani kumkalisha miaka yote hiyo pasipo kusikilizwa,” alisema.
Alisema yeye amekaa huko kwa muda mfupi lakini amepata shida sana kuyazoea mazingira hayo, kwani huwezi kuishi kama nyumbani, hivyo ni vizuri ukiwekwa utaratibu mtu anasomewa kesi yake kwa muda gani.
Lulu alilazimika kukaa gerezani kwa muda huo kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa nguli wa filamu nchini, Steven Kanumba, aliyefariki dunia nyumbani kwake Sinza Vatican Aprili 7, mwaka jana
Related Post:
Wosia wa Mandela watangazwa Johannesburg. Wosia wa aliyekuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela umes… Read More
JAGUAR ASAINI MKATABA MPYA Mwanamuziki tajiri Charles Njagua Jaaguar amesaini mkataba mpya na kampuni ya Mtech it… Read More
PINDA APOKEA MISAADA YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WA MAGOL WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, amepokea msaada ya mabati, mashuka, vyandarua na biskuti vyenye t… Read More
AISEEE HUYU NDIYO DIAMOND PLATINUMZ BWANA,WAKATI WAKE HUU taarifa za chinichini kwamba single ya ‘number one rmx’ ya Diamond Platnumz ft Davido wa Nigeria … Read More
JUSTIN BIEBER ABUSU ZIWA LA BINTI HADHARANI MSANII asiyeisha vituko kila siku Justin Bieber amezidi kuonesha kuwa yeye ni mtu wa vituko ma… Read More
Posted by Unknown
on Thursday, November 7, 2013,
Add Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Response to "LULU ALONGA NA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA "
Post a Comment