Latest Updates

BEIBY MADAHA KALA SHAVU UINGEREZA


MSANII wa filamu na muimbaji wa bongo fleva nchini Baby Joseph 'Beiby Madaha' amepata 'shavu' la kufanya show nchini Uingereza mwishoni mwa mwezi huu, huku akiendelea kuitangaza bidhaa yake ya manukato yanayozalishwa na kampuni ya muziki ya Candy & Candy iliyopo nchini Kenya.
Ndani ya show hiyo ambayo inatarajia kufanyika Novemba 30, msanii huyo pia atapata nafasi ya kuendelea kuitangaza bidhaa zake ikiwemo manukato pamoja na mifuko ya kubebea vitu mbalimbali ikiwemo CD.
Mwanadada huyo amebainisha  kuwa tangu aingia mkataba na kampuni hiyo ya nchini Kenya ameweza kupiga hatua kwenye kazi yake ya muziki hali ambayo kwake anaona ni njia nzuri ya kufikia maendeleo.
Madaha amedai kuwa ndani ya show hiyo mashabiki wake watapata nafasi ya kupata zawadi ya bidhaa hizo ambapo zitazinduliwa tena nchini humo kabla ya kumaliza show hiyo.
Alieleza kuwa bidhaa hizo ni moja ya kazi zake ambapo bado anajipanga kuendelea kufanya vitu vikubwa zaidi katika biashara na kazi zake za muziki.
Mbali na kuzindua bidhaa hizo hivi karibuni msanii huyo alitoa zawadi za bidhaa hizo kwa baadhi ya mashabiki wake mitaanii ambapo alitoa kwa wanawake na watoto ili kuonesha upendo kwa mashabiki .

0 Response to "BEIBY MADAHA KALA SHAVU UINGEREZA "

Post a Comment