Latest Updates

BATULI AWAJIA JUU WASANII WANAOTOA MATUSI
Mwigizaji Yobnesh Yussuph 'Batuli' ameamua kuwatolea uvivu baadhi ya wasanii wa filamu wanaoandika matusi kwenye mitandao na kuwaambia kuwa badala ya wao kupoteza muda huo kutukana matusi makali kwenye mtandao wangetumia muda huo kufanya Ibada ili wakifa waende peponi kwa Amani ambako wangeweza kupajaza mpaka wengine wakose viti.

“…Ule muda watu wanaoutumia kuandika naneno makali (MATUSI) kwenye instagram (Mtandao wa kijamii) wangekuwa wanautumia kwa ibada peponi kungejaa..” Alisema batuli.

Huku ikiwa bado haijajulikana anamlenga nani moja kwa moja na ujumbe huo baadhi ya wachunguzi wa mambo wamehusisha kauli hiyo na kitendo kilichotokea juzi cha msanii mmoja wa filamu wa kike kuporomosha matusi ya nguoni kwenye mtandao huo maarufu wa kijamii nchini.

0 Response to " BATULI AWAJIA JUU WASANII WANAOTOA MATUSI "

Post a Comment