Latest Updates

Batuli "awa-diss" waigizaji na mashabiki wanaoandika matusi kwenye mitandao ya kijamii


Batuli
Mwigizaji Yobnesh Yussuph maarufu kama batuli ameamua kuwatolea uvivu waigizaji wanaoandika matusi kwenye mitandao na kuwaambia kuwa badala ya wao kupoteza muda huo kutukana matusi makali kwenye mtandao wangetumia muda huo kufanya Ibada ili wakifa waende peponi kwa Amani ambako wangeweza kupajaza mpaka wengine wakose viti.
“…Ule muda watu wanaoutumia kuandika naneno makali (MATUSI) kwenye instagram (Mtandao wa kijamii) wangekuwa wanautumia kwa ibada peponi kungejaa..” Alisema batuli.
Huku ikiwa bado haijajulikana anamlenga nani moja kwa moja na ujumbe huo baadhi ya wachunguzi wa mambo wamehusisha kauli hiyo na kitendo kilichotokea juzi cha mwanadada wa bongomovies kuporomosha matusi makali sana kwenye mtandao huo maarufu wa kijamii nchini.

0 Response to "Batuli "awa-diss" waigizaji na mashabiki wanaoandika matusi kwenye mitandao ya kijamii"

Post a Comment