Latest Updates

Baada ya kushauriwa sana kuhusu kuoa, Shija afunguka na kusema yafuatayo


Baada ya kushauriwa sana kuhusu kuoa, Shija afunguka na kusema yafuatayo

Mwigizaji mkongwe wa bongomovies Deogratius Shija, ameamua kufunguka kuhusu ishu  ya kuoa baada ya kupigiwa sana kelele kila sehemu anapoenda kutokana na umri wake kuonekana ukimtupa mkono na huku akiwa haoneshi hata dalili ya kutaka kuoa na kujenga familia kama ilivyo kwa waigizaji wenzake William mtitu au Cloud 112.
Akiongea kwa simu na bongo movies leo hii, Shija amesema kwa suala la kuoa si la kukurupuka kama watu wengi wanavyowaza ila ni suala la kukaa chini na kumuomba Mungu ili ampatie mke mwema.
Shija amesema kuwa, kwa sasa yupo kwenye maombi maalumu akiomba Mungu ampe mke wa uhakika ili ikiwezekana hapo mwakani atulie na familia yake
Akiongea Zaidi Shija alisema, ashawahi kuwa kwenye mahusioano na wanawake kadhaa hapo nyuma lakini wengi wao waliishia kumuumiza moyo hivyo kwa sasa anahitaji mtu mmoja mwaminifu ili atulie naye
Tags:  Deogratius Shija 

0 Response to "Baada ya kushauriwa sana kuhusu kuoa, Shija afunguka na kusema yafuatayo"

Post a Comment